Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wakiongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bw. Dismas Fuko wamekagua miradi ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) iliyofanywa na TPDC katika Kijiji cha Msimbati, Mtwara.

Miradi hiyo ni ujenzi wa Kituo cha Polisi na Kituo cha afya Kijiji cha Msimbati ambapo Kituo cha Polisi kipo zaidi ya 98% kukamilika na Kituo cha afya kipo 90% kukamilika ili kuanza kutoa huduma kwa Wananchi wa Msimbati. 

Aidha, Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TPDC Bw. Dismas Fuko alisema, “Sisi kama Bodi tunawapongeza kwa hatua kubwa zilizofikiwa, kazi ni nzuri kwa ujumla tuendelee kuzingatia suala la ubora katika utekelezaji wa miradi hii na mingine.”