Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)

TPDC kiungo muhimu utekelezaji wa agenda ya Umeme Africa

Imewekwa: 27 January, 2025
TPDC kiungo muhimu utekelezaji wa agenda ya Umeme Africa

 

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania limeonekana kuwa kiungo muhimu katika kuwezesha agenda ya viongozi wakuu wa Afrika ya Kuhakikisha kaya zaidi ya milioni 300 barani Africa wanapata umeme wa Uhakika.

Hayo yamesemwa na Meneja Uhusiano na Mawasiliano kutoka TPDC wakati akieleza mikakati ya TPDC katika kuleta mageuzi ya nishati nchini na Africa kwa Ujumla wakati akipokea wageni mbalimbali wanaotembelea katika banda la maonyesho ya TPPDC JNICC wakati Mkutano Mkuu wa Nishati wa Wakuu wa Afrika Ukiendela.

“Sisi TPDC pamoja na kugundua kiasi kikubwa cha gesi asilia kipatacho futi za ujezo trillion 57.54 ambayo imeendelea kuwa moja ya vyanzo vikuu vya uzalishaji wa umeme nchini, TPDC limeendelea kazi za utafiti zaidi wa gesi asilia na mafuta, uendelezaji na uzalishaji wa gesi asilia kwa lengo la kuongeza kiasi cha gesi asilia ili kuwezesha matumizi yake katika uchumi,” ameeleza Bi. Marie.

Aidha Bi. Marie amefafanua kuwa TPDC kwa kushirikiana na kampuni yake tanzu ya GASCO linaendelea na ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya kusambaza na kusafirisha gesi asilia nchi kwa ujenzi wa miundombinu ya mabomba, ujenzi wa kituo mama cha CNG, vituo vya kuhamishika na malori ya kusafirishia gesi asilia nchini ili kuwezesha upatikanaji wa gesi asilia katika maeneo mbalimbali ya nchi nchini kwa matumizi ya uzalishaji wa umeme, viwanda na n.k.

TPDC imeendelea kushirikisha kampuni binafsi ili kuweza kujenga mitambo midogo ya kubalidi gesi asilia kuwa kimiminika ambapo tayari kampuni kadhaa zimeshaingia makubaliano ya awali na TPDC.