Kamishna wa Polisi wa Operesheni na Mafunzo Awadhi Juma Haji ametembelea na kukagua kituo cha kupokea gesi asilia Kinyerezi Jijini Dar es salaam na kituo cha makutano ya awali ya kupokea gesi asilia kilichopo Somangafungu Kilwa Mkoani Lindi tarehe 24/01/2023.
Akiwa katika ziara hiyo amewaasa Makamanda wa Jeshi la Polisi wanaosimamia maeneo ya mkuza wa bomba la gesi asilia kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kuzingatia kanuni na misingi ya kiutendaji ya Jeshi la Polisi kwa manufaa ya Wananchi na Taifa .
Katika ziara hiyo ya Kikazi CP Awadhi ameambatana na Makamanda wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, Makamanda wa Wilaya zinazopitiwa na bomba la gesi katika Mikoa ya ( Mtwara,Lindi na Dar es salaam), Kaimu Meneja wa Kampuni Tanzu ya GASCO Bw. Elisamehe Macha, Mkuu wa Kitengo cha Usalama GASCO Bw.Fred Mfikwa pamoja na Maafisa wa TPDC.
Ziara hiyo ni muendelezo wa ziara aliyoianza tarehe 23/01/2023 kwa kukagua kiwanda cha kuchakata gesi asilia kilichopo kisiwani SongoSongo Mkoani Lindi.
- By:Beatrice Peter
- 0 comment