Kwa mwaliko wa Serikali ya Indonesia, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC Mhe. Balozi Ombeni Sefue, alihudhuria Kongamano la Indonesia-Afrika mjini Bali Indonesia. Pamoja na kushiriki katika mjadala na Viongozi wengine, Balozi Sefue pia alishiriki katika hafla ya makabidhiano ya Hati ya Makubaliano (MOU) kati ya TPDC na PERTAMINA inayoongeza muda wa ushirikiano kati ya Kampuni hizo mbili kuendelea kushirikiana katika kujenga uwezo pamoja na kutafuta fursa za uwekezaji nchini Tanzania.
- By:Beatrice Peter
- 0 comment