Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Ndg. Msafiri Mbibo amelipongeza Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa namna linavyotekeleza Miradi yake kwa kutumia Wataalam wa ndani katika utafiti wa miradi ya mafuta na gesi.
Pongezi hizo amezitoa wakati alipotembelea katika banda la TPDC kwenye Mkutano Mkuu wa Wajiolojia unaofanyika Jijini Tanga ambapo alikua mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano huo uliofanyika tarehe 04 Desemba,2024.
Akiwa katika banda la TPDC aliweza kupewa maelezo ya Miradi mbalimbali inayotekeleza na Shirika ukiwemo Mradi wa utafutaji wa mafuta na gesi inaotekelezwa katika Kitalu cha Eyasi Wembere, mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), mradi wa LNG pamoja na miradi ya usambazaji wa gesi asilia viwandani, majumbani na kwenye magari.
- By:Beatrice Peter
- 0 comment