TPDC Yaendesha Zoezi La Utoaji Elimu Ya Miundombinu Ya Gesi Asilia Lindi

TPDC Yaendesha Zoezi La Utoaji Elimu Ya Miundombinu Ya Gesi Asilia Lindi

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeendesha zoezi la utoaji elimu kwa
Wananchi wa Vijiji/Mitaa inayopitiwa na miundombinu ya gesi asilia.Shirika limekua na
utaratibu wa kutoa elimu kwa umma juu ya miradi mbalimbali ya utafiti na uendelezaji
wa nishati ya mafuta na gesi asilia nchini. Elimu hii imetolewa ikiwa ni sehemu ya
kuimarisha mahusiano mazuri na kuwajengea uwezo wananchi kutambua fursa za
uwekezaji wa miradi ya gesi pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama wa miundombinu
ya bomba la gesi asilia .
Zoezi hilo limefanyika Mkoani Lindi kupitia mikutano ya hadhara katika Vijiji ambavyo
vimepitiwa na mradi wa bomba la gesi asilia ambapo elimu hiyo ilijikita kwenye mada za
ulinzi na usalama, fursa zinazoambatana na miradi ya gesi asilia (manufaa) pamoja na
Uwajibikaji wa Shirika kwa Jamii (CSR).
Akizungumza katika moja ya mikutano na wananchi wa Kijiji cha Somanga Kusini, Afisa
Maendeleo ya Jamii wa TPDC Bw. Oscar Mwakasege ameeleza kuwa utunzaji na
usalama wa mradi wa bomba la gesi asilia nchini ni pamoja na ushirikishwaji wa
wananchi katika ngazi zote hususani katika kupata taarifa, elimu, utekelezaji wa miradi
ya kijamii pamoja na ushirikishwaji kwenye ulinzi na usalama.
‘’Mradi wa bomba la gesi asilia umekua na manufaa makubwa kwa jamii na Taifa kwa
ujumla ambapo mpaka sasa 70% ya umeme nchini unazalishwa kwa kutumia gesi asilia
hivyo kuchagiza ukuaji wa Sekta mbalimbali, kadhalika gesi asilia inatumika
kuendeshea mitambo viwandani ambapo viwanda vipatavyo 53 na nyumba takribani
1500 za Mikoa ya Dar es salaam, Mtwara na Lindi (Mnazi mmoja) zimeunganishwa
katika mtandao wa gesi asilia kwa matumizi ya kupikia majumbani, aidha mpaka sasa
zaidi ya magari 1500 yanatumia gesi asilia kama nishati mbadala wa petroli na dizeli.
Katika hatua nyingine Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Usalama TPDC Bw.Fredy Mfikwa
alieleza kuwa mradi wa bomba la gesi asilia umegusa Vijiji na Mitaa 139 kuanzia
Msimbati Mtwara hadi Dar es salaam. Aidha, alieleza kuwa TPDC inashirikiana vizuri na
Vijiji/Mitaa hiyo kwenye suala la ulinzi na usalama ikiwa ni pamoja na kutoa fedha kila
mwezi kwa kila Kijiji/Mtaa ili kuwezesha vijiji hivyo kufanya usafi kwenye njia (Mkuza)
wa bomba la gesi asilia.
Bw.Mfikwa alitoa rai kwa wananchi kuendelea kuitunza miundombinu ya bomba la gesi
asilia kwa kuacha kufanya shughuli hatarishi za kibinadamu ndani ya miundiombinu
hiyo, pamoja na kuwasisitiza wananchi kuendelea kutoa taarifa kwa uongozi wa
Vijiji/Mitaa au TPDC pindi wanapoona mazingira hatarishi ndani ya miundombinu ya
bomba la gesi asilia.
‘’Shughuli za kibinadamu ambazo hazipaswi kufanywa ndani ya Mkuza wa bomba la
gesi asilia kama kuchimba mchanga, kilimo cha mazao ya muda mfupi na mrefu,
kuchoma nyasi moto, kupitisha makundi makubwa ya mifugo na shughuli zozote za
ujenzi haiziruhusiwi, hivyo natoa rai kwa Uongozi wa Vijiji na wananchi kuendelea

kudumisha ulinzi na usalama ili bomba hili liendelee kuwa na manufaa kwa sasa na
baadae,’’ alieleza Mfikwa.

miradi ya mbalimbali ikiwemo kuzalisha umeme ambapo zaidi ya asilimia 70% ya
umeme unaozalishwa katika gridi ya Taifa unatokana na gesi asilia, kadhalika gesi
asilia inatumika kuendeshea mitambo viwandani ambapo viwanda vipatavyo 53 na
nyumba takribani 1500 zimeunganishwa katika mtandao wa gesi asilia kwa matumizi
ya kupikia majumbani, aidha mpaka sasa zaidi ya magari 1500 yanatumia gesi asilia
kama nishati mbadala wa petroli na dizeli.