Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi TPDC wamepongeza jitihadaa zinazofanywa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika kuwajengea uwezo wafanyakazi wanaoendesha mitambo ya kuchakata gesi asilia Songosongo na Madimba ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya muda na muda mrefu ndani na nje ya nchi. Mkakati huu imewezesha wafanyakazi hao kuwa na uwezo mkubwa wa kuendesha mitambo hiyo kwa ufanisi wa hali ya juu.

Akiongea baada ya ziara hiyo, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Mjiolojia Salvatory Ntomola alisema ‘‘ni jambo la kujivunia kwa TPDC na Nchi kuona mitambo hii ikiendeshwa na Watanzania kwa asilimia mia moja’’.