Hayo yameelezwa katika ziara ya Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) inayoongozwa na Mhe. Balozi Ombeni Sefue wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya TPDC iliyopo TIPER Kigamboni leo tarehe 07/6/2024.

Lengo la ziara hiyo ni kujionea hali halisi ya miundombonu ya miradi ambayo kwa muda mrefu imekua haitumiki pamoja na kueleza mikakati iliyopo ya ukarabati na ujenzi wa miundimbinu mingine mipya ili nchi iwe na uwezo mkubwa wa kuhifadhi mafuta. 

 Akieleza mipango ya TPDC katika kuhakikisha nchi inakua na hifadhi kubwa ya mafuta Sefue amesema kuwa, ‘‘kwa sasa tayari mchakato wa ukarabati wa Tanki Namba 8 lenye uwezo wa kuhifadhi tani za   ujazo 45,000 umeshaanza’’

Halikadhalika, TPDC inakusudia kujenga matanki mengine sita yenye uwezo wa kuhifadhi tani za ujazo 162,000 kwa Mkoa wa Dar es salaam, mikoa mingine ni Dodoma na Mwanza. 

Aidha, ilielezwa kuwa ukarabati wa Tanki Namba 8 unakusudiwa kuanza mwezi wa Juni,2024 na kumalizika ndani ya miezi ishirini.

Miundombinu ya TPDC iliyopo eneo la TIPER ilijengwa mwaka 1993, miundombiu hiyo ni Tanki namba 8, mitambo ya  Kuchakata, kutunza na kupakia lami.