Uwajibikaji wa kijamii wa Shirika letu (Corporate Social Responsibility - CSR) ni sehemu ya msingi ya namna tunavyoendesha shughuli zetu.
Tunalenga kuleta athari chanya katika jamii tunazofanyia kazi, kwa kuhakikisha kuwa shughuli zetu zinachangia katika maendeleo ya uchumi wa maeneo husika na kuboresha kipato cha kaya pamoja na ubora wa maisha kwa wananchi.
Jitihada zetu za uwajibikaji wa kijamii haziishii tu katika maeneo ya kazi, bali pia zinaenea katika jamii kwa ujumla kupitia uwekezaji kwenye elimu, afya, na miradi ya kuwawezesha wananchi kupitia programu mbalimbali za Uwajibikaji wa Kijamii kwa Jamii (CSR).