>
emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania
ega Logo
Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
svg-tree

❓ Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

Ni kweli BG imenunuliwa na Shell ununuzi huo pia umehusu maeneo ya Gesi asilia ya Tanzania. Kama sheria inavyosema makampuni yote ya gesi Tanzania yakiuza hisa zake lazima walipe kodi kwa serikali kwa usimamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kwanza, Shirika halina uhakika kama Serikali iliagizwa kuwapunguza wafanyakazi wa TPDC mwaka 1986 kama unavyodai.

Pili, Kwa kujibu swali lako TPDC haina taarifa ya uwepo wa wataalam hao 100 wa Tanzania katika nchi za jirani.  Hata hivyo, nafasi za kazi zikitokea TPDC huwa zinatangazwa kwenye vyombo vya habari nje na ndani ya nchi na kwenye tovuti mbalimbali. Wataalam hao kama wapo wanashauriwa kuomba nafasi hizo mara tu zinapotangazwa.

Kwanza, Faida kubwa zaidi ya kukamilika kwa bomba hili la Gesi asilia ni upatikanaji wa umeme wa uhakika na wa bei nafuu ukilinganishwa na ule uliokua unazalishwa kwa kutumia Mafuta. Kwa sasa mchango wa Gesi asilia kwenye uzalishaji na upatikanaji wa umeme nchini ni zaidi ya asilimia 70%.

Pili, Ukuaji wa sekta ya viwanda ambao kwa kiasi kikubwa umechochewa na upatikanaji wa Nishati nafuu ya uhakika iwe kwa kupitia umeme ambayo 70% unatokana na Gesi asilia ama kwa matumizi ya gesi asilia moja kwa moja. Uthibitisho unaonekana wazi mpaka sasa viwanda 52 vimeunganishwa na matumizi ya gesi asilia asilia katika mikoa ya Pwani, Lindi, Mtwara na Dar es Salaam.

Tatu, Matumizi ya Gesi asilia kwa kupikia majumbani na matumizi ya Gesi asilia kwa kupikia kwenye Taasisi ambapo tayari Mikoa ya Dar es Salaam na Mtwara imeshaanza kunufaika na ujenzi wa utanuzi wa miundombinu ya usambazi wa gesi asilia unaendelea wakati huo tafiti na upembuzi yakinufu unandelea katika mkoa wa Lindi. Matumizi ya Gesi asilia majumbani yameendelea kuongezeka kulingana na kuendelea kwa ujenzi wa miundombinu ya Gesi asilia unaofanywa na TPDC na kampuni tanzu GASCO katika mikoa ya Mtwara na Dar es Salaam. Zaidi ya nyumba 500 katika Mkoa wa Mtwara zimeunganisha na Gesi asilia hadi kufikia Februari 2022, wakati kwa Mkoa wa Dar es Salaam hadi sasa sasa ni nyumba zaidi ya 1500 zinatumia Gesi asilia. Aidha ujenzi wa miundombinu ya kusambaza gesi asilia ni endelevu.

Nne, Upatikanaji wa Ajira za kudumu na Ajira za muda mfupi moja kwa moja kwenye viwanda na mitambo ya uzalishaji wa umeme, mitambo ya kuchakata na kusafirsha gesi asilia pamoja na vituo vyake vya Madimba-Mtwara, SongoSongo na Somanga-Lindi pamoja na Kinyerezi Dar es Salaam. Ukuaji wa ajira zitokanazo na huduma kama vile usafirisha, malazi, kibenki na ukuaji wa biashara, uvuvi, kilimo na ufugaji.

Tano, Ukuaji wa uchumi na uboreshwaji wa huduma za kijamii.

Sababu za kujenga miundombinu ya bomba la Besi asilia kutoka Mtwara na Lindi kwenda Dar es Salaam limegawanyika katika vipengele vifuatavyo:

Kwanza, Kabla ya kujenga miundombinu hiyo kuliangaliwa uhitaji mkubwa wa Gesi asilia ulipo nchini, kwa ajili ya viwanda, kuzalisha umeme n.k.  Aidha, ilionekana kwamba viwanda vingi na mahitaji mengi tayari yapo katika Jiji la Dar es salaam ambalo ni jiji la biashara

Pili, Uwepo wa miundombinu ya bomba la gesi kwenda Dar es Salaam hauzuii fursa kwa Mikoa ya kusini kutokunufaika na Gesi asilia. Itakumbukwa kwamba Mkoa wa Mtwara ulianza kunufaika na Gesi asilia toka mwaka mwaka 2006 baada ya kukamilika kwa mradi wa Gesi asilia unaotoka Mnazibay hadi Mtwara, kwa ajili ya kuzalisha umeme na kuwezesha matumizi mengine.

Mkoa wa Lindi nao ulianza kunufaika na gesi asilia mwaka 2004 kutokana na bomba la Songas ambalo moja ya manufaa yake ni uzalishaji wa umeme unaotumika katika Mkoa huo.

Tatu, Kwa upande wa bomba la gesi asilia linalosafirisha na kusambaza gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, limejengwa kimkakati ili kuhakikisha gesi asilia inaweza kutumika katika kila mkoa linapopita kwa kuwekewa maeneo wezeshi kwa usambazaji. Ili kuthibitisha hili tayari Kiwanda cha Saruji cha Dangote kinatumia gesi asilia kutoka kwenye bomba hili.

Nne, Mikoa ya Lindi na Mtwara pia inanufaika kupitia malipo ya mrabaha Pesa ambazo zinasaidia Halmashauri pamoja na majukumu mengine kuwezesha uboreshwaji wa huduma za kijamii zikiwemo za afya, elimu na miundombinu.

Tano, Mikoa ya Lindi na Mtwara ndio wanufaika kubwa wa ushiriki wa makampuni ya mafuta na gesi likiwemo TPDC katika uboreshwaji wa huduma mbalimbali za kijamii.

Kwa mantinki hiyo, uwepo wa Nishati hii ya Gesi asilia kunatoa pia fursa ya kunufaika kwa mikoa ya Lindi na Mtwara.

 

 

 

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzani (TPDC) ni Taasisi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Shirika linapokuwa na uhitaji wa wafanyakazi kama yalivyo mashirika mengine ya serikali hufuata sheria, taratibu na miongozo ya Utumishi wa Umma kupitia Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Taratibu zote za kuajiri watumishi wa umma hufuatwa ikiwa ni pamoja na kuzingatia sifa za waombaji, uzoefu, weledi wa utendaji wao na Taaluma zao.

Hili halina ukweli wowote! Tangu matokeo ya gunduzi za miaka ya hivi karibuni kutolewa kumekuwepo na upotoshaji wa taarifa zisizo sahihi kwa wananchi, kwamba, watapatiwa fedha taslimu kupitia mitandao ya simu, mabenki, hata ikiwemo kuwapatia fedha taslimu Mifukoni mwao.
Katika hili ukweli ni kwamba wananchi watanufaika na rasilimali hii kwa namna tofauti, baadhi kupata ajira za muda mfupi au za kudumu, wapo watakaotoa huduma na kuuza bidhaa katika sehemu za miradi ya Gesi asilia. Aidha, Gesi asilia itakuwa nishati ya kuzalishia umeme wa uhakika kwa matumizi viwandani, majumbani na kwenye magari.

 

Tangu ugunduzi wa gesi asilia uanze kufanyika katika maeneo ya Songo Songo mkoa wa Lindi na Mnazi Bay katika Mkoa wa Mtwara, kumekuwepo na mabadiliko chanya katika Mikoa hiyo. Mchango wa Shirika katika Mikoa hiyo umegawanyika katika sehemu zifuatazo;

Kwanza, Kumekuwepo na mchango wa ukuaji wa uchumi kutokana na uwepo wa umeme wa uhakika ambao huzaishwa kwa kutumia Gesi asilia katika Mikoa hiyo.

Pili, Matumizi ya Gesi asilia kwa kupikia majumbani na kwenye taasisi mbalimbali ambapo Mkoani Mtwara hadi kufikia 2022 nyumba zaidi ya 500 na Taasisi nane zimeunganshwa na kuanza kutumia gesi asilia, zoezi hili ni endelevu na Shirika linakusudia kuunganisha Nyumba na Taasisi nyingi zaidi. Matumizi haya ya gesi asilia yanakwenda sambamba na unafuu wa bei ya Gesi asilia, urafiki wa Nishati hii kwa Mazingira na uhakika wa upatikanaji wake.

Tatu, Matumizi ya Gesi asilia Viwandani ambapo kwa Mkoa wa Mtwara kiwanda kikubwa cha Cement cha Dangote kimeshaanza kutumia gesi asilia kama nishati ya kuzalisha umeme na kuendeshea mitambo, na kwa matumizi ya kuendeshea magari.

Nne, Faida nyingine ya Gesi asilia kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara ni pamoja na; ajira za kudumu za muda mfupi na mrefu katika Viwanda na kwenye miradi mbalimbali ikiwemo ya usambazaji wa Gesi asilia, upatikanaji wa fursa za kibiashara, fedha inayookolewa kwa kutumia Gesi asilia hutumika kwa matumizi mengine.

Tano, Mikoa ya Lindi na Mtwara imekua ikipata mrabaha unatokana na uwepo wa gesi asilia katika maeneo hayo.

Sita, Shirika kwa kushirikiana na makampuni ya mafuta na gesi nchini wamekuwa wakisadia shughuli za kijamii kama, afya, elimu, miundombinu, Miradi ya maji, utawala bora pamoja na michezo katika kuboresha maisha ya Wananchi wa Mikoa hiyo.

Kama gesi asilia ikiuzwa nje ya nchi, Je kiasi kitakacho salia kinaweza kutosheleza matumizi ya ndani ya nchi?

Jibu:

Hadi kufikia sasa 2022 kiasi cha gesi asilia kilichogunduliwa Nchini ni jumla ya futi za ujazo tilioni 57.54.

Kiasi hiki ni kikubwa na cha kutosheleza, inakadiriwa kwamba kiasi hiki kinaweza kutosheleza hata kama itauzwa nje ya nchi bado mahitaji ya ndani hayataathirika.

Taarifa hii si sahihi. Ukweli sahihi ni kwamba kupitia mradi wa TLNG (Tanzania Liquified Natural Gas-Gesi asilia kimimika) gesi asilia iliyopo kwenye kina kirefu cha bahari ili iweze kusafirishwa lazima ibadilishwe iwe kwenye hali ya kimiminika na mitambo ya kubadilisha gesi kuwa kimiminika itajengwa eneo la Likong’o mkoani Lindi.

Serikali inatekeleza Miradi 9 ya kimkakati katika mpango wa Maendeleo wa 2025, kati hiyo miradi minne inasimamiwa na kutekelezwa na TPDC. a. Mradi wa kwanza ni wa utafutaji wa mafuta katika kitalu cha Eyasi Wembere Mradi huu ni moja ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali kwa kupitia TPDC, mradi huu umelenga kugundua Mafuta na hivyo kutekeleza jukumu la utafutaji mafuta la Shirika. Hadi sasa tayari tafiti mbalimbali za ukusanyaji taarifa za kijiolojia na kijiofzikia zimekwisha fanyika na vipo viashiria kwamba mafuta yanaweza kupatikana, hii ni kutokana na Jeolojia ya Eneo la Eyasi kufanana na ile ya lake Albert Uganda ambapo wameweza kugundua mafuta, na ile ya Turkana nchini kenya ambapo napo Mafuta yamepatikana. b: Mradi wa pili ni wa kusindika gesi asilia kuwa kimiminika-TLNG. Mradi huu unalenga kusindika Gesi asilia kutoka kwenye kina kirefu cha Bahari ili kuwezesha kuuza Gesi hiyo nje na ndani ya Nchi. Mradi huu utahusisha Gesi asilia iliyogunduliwa katika Vitalu namba 1, 2 na 4 vilivyopo katika kina kirefu cha Bahari. Hadi kufikia sasa Eneo la Mradi (Likong’o-Lindi) limeshapatikana na fidia kwa Wananchi watakaopisha Mradi imefanyika. Serikali kupitia TPDC imekamilisha majadiliano ya kimkataba (HGA negotiations) na wawekezaji wa Mradi. c: Mradi wa Tatu ni wa Utafutaji wa mafuta na Gesi asilia katika kitalu cha Mnazi-Bay Kaskazini. Kufikia 2024 Serikali kupitia TPDC imepanga kuchoronga visima viwili katika kitalu hiki. Kisima kimoja kitakuwa cha utafiti na kingine cha uendelezaji wa Gesi asilia. Taarifa za awali zimeonesha uwepo wa mashapo yenye uwezekano wa kuwa na gesi asilia. Kazi ya kuandaa mpango wa kuchoronga visima vya utafutaji na uendelezaji katika mashapo yaliyobainishwa imekamilika. Pindi ugunduzi wa gesi asilia katika kitalu hichi ukifanyika, gesi hiyo itaongeza kiwango cha gesi asilia kilichopatikana hapa nchini ambacho kitawezesha upatikanaji wa Nishati ya kutosha na kukuza maendeleo ya Viwanda hapa Nchini. d: Mradi wa nne ni wa Bomba la kusafirisha mafuta ghafi la Afrika Mashariki-EACOP. Mradi huu unahusu ujenzi wa Bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania. Bomba hili lenye urefu wa Kilomita 1447 kati ya hizo 1149 zipo nchini Tanzania ambapo limepata kwenye Mikoa Nane, Wilaya 24 na Kata 134. Faida za Bomba hili kwa nchi yetu ni pamoja na; usihiriki wa watanzania katika kutoa huduma mbalimbali, kodi za Serikali, tozo, ajira, na ushiriki wa watanzania katika mradi. Je, Ni kweli kwamba makampuni ya mafuta na gesi yaliyo gundua Gesi asilia katika kina kirefu cha Bahari yameshaanza kuvuna gesi asilia na kusafirisha nje ya nchi? Jibu: Makampuni ambayo mpaka sasa yamefanikiwa kufanya ugunduzi wa Gesi asilia katika tafiti za mafuta na gesi kwenye kina kirefu cha bahari hapa nchini ni Shell, Equinor pamoja na washirika wake, lakini bado hawajaanza kuvuna Gesi asilia na kusafirisha nje ya nchi.

TLNG maana yake ni Tanzania Liquefied Natural Gas, yaani gesi iliyobadilishwa kuwa kimiminika kwa njia ya kupooza kwenye joto la -162 degree centigrade. Lengo kuu la kubadilishwa kuwa kimiminika ni kupunguza ujazo, yaani kwa uwiano wa 1/600. Kama gesi ilitakiwa kubebwa kwa meli 600, ikibadilishwa na kuwa kimiminika itabebwa na meli moja tu.

Mradi huu ni miongoni mwa miradi ya kimkakati (Strategic project) utaendeshwa kwa ubia (Special purpose vehicle) ambapo washiriki wake ni wabia wa kitalu namba 1 na 4 (TPDC, Shell, Pavillion na Ophir) pamoja kitalu namba 2 (TPDC, Equinor na Exxonmobil).

Miundombinu itakayojengwa ni mitambo ya kuchakata gesi kuwa kimiminika na Mabomba ya kutoa gesi Baharini na kuchimba Visima vya uzalisharishaji Baharini.  Ujenzi wa mitambo hiyo utafanyika Mkoani Lindi eneo la Likong'o na Mtomkavu. TPDC ndiye mmiliki wa leseni zote za Vitalu, hivyo atashiriki kwenye miradi ya kuchimba (upstream) na pia atashiriki kwenye mradi wa TLNG kwa niaba ya Serikali. Pia atakuwa msimamizi wa mgao wa mapato ya uzalishaji gesi kwa niaba ya Serikali (Royalty na Profit gas).

Mradi huu unatarajiwa kugharimu dola za Marekani takribani bilioni 30 ikijumuisha na visima na mabomba ya kusafirisha gesi hadi nchi kavu. Kiasi cha futi za ujazo takribani 25 trillion zitatumika na zitatoka bahari ya kina kirefu. Muda wa ujenzi wa mradi huu ni miaka 4 hadi 5.

Baada ya ujenzi kukamilika, makadirio ya maisha ya mitambo na uwepo wa Gesi asilia, unakadiriwa kuchukua zaidi ya miaka 30 baada ya ujenzi.

Manufaa ya mradi huu ni kama vile; kuongeza kiwango cha gesi asilia kwa matumizi ya ndani ya Nchi, kuchochea ukuaji wa sekta ya Viwanda, kuongeza uwekezaji wa ndani na wa nje, uboreshwaji wa Huduma za jamii na miundombinu wezeshi ya ukuaji wa uchumi wa nchi, ongezeko la ajira, kuliongezea taifa pesa za kigeni n.k.

Mpangilio