TPDC inaamini kuwa mafanikio yetu yanahusiana kwa karibu na ustawi wa wafanyakazi wetu, wateja, na jamii tunazofanyia kazi.
Tamko letu la Sera ya Afya na Usalama Kazini (OHS Policy Statement)(hapa weka kiungo cha sera) limelenga kuimarisha utamaduni wa usalama kazini kwa kuhakikisha hakuna madhara yoyote kwa watu wala jamii za maeneo tunayofanyia kazi.
Tunakuza utamaduni wa usawa na utofauti katika ngazi zote za Shirika na Kampuni tanzu zake.
Tunatekeleza programu za Afya na Usalama Kazini (OHS) zinazounga mkono fursa sawa za ajira, maendeleo ya taaluma, na afya ya mwili kwa wafanyakazi wetu.
Tumejizatiti kuhakikisha mazingira ya kazi ni salama na yenye heshima, ambapo afya na usalama wa wafanyakazi wetu ni jambo la kipaumbele.
Kama Shirika la Taifa la Mafuta, tunazingatia Kanuni Tisa za Kuokoa Maisha (Nine Life Saving Rules) ambazo zilibuniwa ili kuzuia ajali mbaya na majeraha makubwa kwa kuelekeza hatua za msingi za kiusalama zinazopaswa kuchukuliwa katika mazingira yenye hatari kubwa.
Kanuni hizo Tisa za Kuokoa Maisha ni pamoja na: