Shirika limejikita katika kupunguza athari za kimazingira kwa kutumia mbinu za uwajibikaji na usimamizi bora wa rasilimali. Lengo letu ni kupunguza kiwango cha hewa ya ukaa (carbon footprint), kutekeleza miradi ya nishati endelevu, na kuendeleza matumizi ya nishati safi kwa ajili ya kupikia.
Shughuli zetu zote zinaendeshwa kwa kuzingatia Sera ya Usimamizi wa Mazingira (Environmental Management Policy) (hapa weka kiungo cha sera hiyo).
Aidha, tumejielekeza katika kuendeleza miundombinu ya gesi asilia inayolenga kuimarisha usalama wa upatikanaji wa nishati na kuongeza upatikanaji wa nishati kwa wananchi, sambamba na kuchangia katika maendeleo ya uchumi wa Taifa na ngazi za chini.
Kwa kufanya hivyo, tunahakikisha malengo yetu ya maendeleo endelevu yanahusiana moja kwa moja na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (UN-SDGs), Ajenda 2063 ya Afrika, pamoja na Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050