Kuna tofuti kubwa kati ya gesi asilia na gesi ya mitungi. Tofauti zake ni kama zifuatazo: -
Gesi asilia ni zao la masalia ya wanyama na mimea vilivyoishi na kuoza na hatimaye kutengeneza mwamba tabaka. Gesi ya mitungi ni mabaki ya mifuta.
GESI ASILIA | GESI INAYOHIFADHIWA KWENYE MITUNGI (LPG |
Kikemia Gesi asilia ni mchanganyiko wa Gesi mbalimbali kama methane zilizotokea kutokana na kuoza kwa mata ogania kama mimea kwa Miaka mingi iliyopita. | LPG ni mchanganyiko wa Hydrocarbon Zaidi ya moja hasa propane na butane na huhifadhiwa katika hali ya kimiminika. |
Hupatikana mojamoja toka kwenye miamba ardhini. | Hupatikana wakati uzalishaji wa mafuta yanayotumika kwenye magari (Petroli na Dizeli) au wakati wa uzalishaji wa Mafuta na Gesi. |
Gesi hii ni nyepesi kuliko hewa na hivyo ina uwezo wa kutawanyika hewani pale inapotokea imevuja na usalama wake ni wa uhakika. | Ni nzito kuliko hewa na pale inapovuja haitawanyiki umbali mrefu. |
Husafirishwa/kusambazwa kwa njia ya Mabomba, na kama itasindikwa itasafirishwa kwa meli maalum za LGN (Liquefied Natural Gas) ama CNG (Compressed Natural Gas) | Huhifadhiwa katika hali ya kimiminika kwenye matenki au mitungi |
Kuanzia mwaka 1977 hadi 1999 TPDC ndiyo alikuwa mwagizaji pekee wa bidhaa za petroli nchini. Ilipofika Januari 2000, sekta ndogo ya petroli ilifanywa kuwa huria na kuruhusu makampuni binafsi ya petroli kuagiza bidhaa za petroli na hivyo kuiondoa TPDC katika biashara ya mafuta. Mbali na uingizaji wa mafuta ghafi na bidhaa zake, TPDC pia ilikuwa ikitekeleza majukumu ya udhibiti ikiwa ni pamoja na kupanga bei na kusimamia biashara ya mafuta ya petroli.