TPDC Yaendesha Semina Kwa Waandishi Wa Habari

Waandishi wa Habari wamekumbushwa kutumia vyema taaluma yao kuisemea Sekta
ya mafuta na gesi asilia nchini ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika Uchumi
wa Taifa
Hayo yamesemwa na Meya wa Manispaa ya Morogoro Mhe. Paschal Kihangi wakati
wa ufunguzi wa semina ya Waandishi wa Habari kuhusu Sekta ya mafuta na gesi asilia
Mkoani Morogoro
Semina hiyo imeandaliwa na Shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ikiwa na
lengo la kuwajengena uwezo wa kujua Miradi ya kimakakati inayosimamiwa na Shirika
hilo.
Akizungumza wakati wa semina hiyo Mhe. Kihangi amesema Waandishi wa Habari ni
kundi muhimu nchini na kupitia wao wananchi wanapata taarifa sahihi kwa wakati
kuhusu fursa mbalimbali na kuelewa Miradi ya utafutaji na uendeshaji wa rasilimali ya
mafuta na gesi.
Aidha, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kutoka TPDC Bi. Marie
Msellemu, amesema semina hiyo ni muendelezo wa semina mbalimbali ambazo
zimekuwa zikitolewa kwa Wadau ili kuwajengea uwezo wa kujua Miradi ya kimakakati
kwa nchi hasa iliyopo chini ya TPDC.
Serikali inaendelea kutekeleza Miradi 19 ya kimkakati huku Miradi 9 ikiwa Wizara ya
Nishati na Miradi 4 inasimamiwa na TPDC.
Miradi hiyo ni pamoja na Mradi wa kusindika gesi asilia kuwa kimiminika (LNG), Mradi
bomba la kusafirisha mafuta ghafi Afrika Mashariki (EACOP), utafutaji wa mafuta Bonde
la Eyasi Wembere na Mradi wa utafutaji wa gesi asilia Kitalu cha Mnazi Bay Kaskazini.