Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) leo tarehe 31/08/2023 limezikabidhi rasmi Kampuni zake Tanzu za GASCO na TANOIL miongozo na Sheria mbalimbali zitakazowaongoza katika utekelezaji wa majumu yao mapya.

Aidha, Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC, Balozi Ombeni Sefue amewaasa Wenyeviti na Wajumbe wa Bodi hizo kutafsiri malengo ya Shirika mama (TPDC) yaliyotolewa na Serikali na kuhakikisha Menejimenti za Kampuni hizo zinatekeleza Majukumu yao kwa ufanisi na kuleta faida katika shughuli mahususi za Kampuni Tanzu hizo ili kuhakikisha adhma ya kuifanya TPDC na Makampuni Tanzu hayo yanajiendesha Kibiashara na Kiushindani.