Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Bw. Mussa Makame amefanya kikao na Wafanyakazi wa TPDC HQ, GASCO na TANOIL.Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 15/03/2023 Jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika kikao hicho Bw. Makame amesema Shirika limepata mafanikio mengi katika mwaka 2022, ambapo miradi mbalimbali ipo katika hatua nzuri ya utekelezaji. Miradi hiyo ni mradi wa utafutaji wa mafuta na gesi Kitalu cha Mnazi Bay Kaskazini na Kitalu cha Ruvuma, mradi wa kusindika gesi asilia kuwa kimiminika (Liquified Natural Gas) ambapo majadiliano yamekamilika,mradi wa bomba la  kusafirisha mafuta ghafi Afrika Mashariki (EACOP), biashara ya CNG (Compressed Natural Gas) na Biashara ya uingizaji mafuta.

Aidha Bw.Makame amewasisitiza wafanyakazi kuendelea kufanya kazi kwa bidii, ushirikiano, weledi na ufanisi.

Kikao hicho kimeenda sambamba na utolewaji wa mafunzo ya VVU na Ukimwi kwa Wafanyakazi.