Maafisa wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), wamefanya mkutano wa kutoa elimu kuhusu matumizi ya gesi asilia kwa Wananchi wa Kata ya Mnazi Mmoja mkoani Lindi.

Lengo la mkutano huo lilikuwa ni kuwahamasisha wananchi wa maeneo hayo waliopitiwa na bomba la gesi kuwa na utayari wa kununua majiko ya gesi ili waweze kuunganishiwa gesi asilia kwenye nyumba zao kwaajili ya matumizi.

Katika eneo hilo jumla ya nyumba 209 zinatarajiwa kuunganishwa na mtandao wa gesi asilia ikiwa shughuli za awali za kulaza bomba kutoka BVS 3 iliyoko Kijiji cha Maumbika hadi eneo la Mnazi Mmoja umekamilika kwa zaidi ya 90%.