Our Latest Blog Posts
13
Sep

NCHI NNE MBIONI KUNUFAIKA NA GESI ASILIA TANZANIA 

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limesema tayari limeingia makubaliano na Kampuni mbili za kigeni kwa ajili ya ujenzi wa mitambo ya kisasa ya kusafirisha gesi asilia katika nchi ya Uganda, Congo,Kenya na Zambia. Kampuni ambazo zimeingia makubaliano na TPDC Mei 2024 ni ROSETTA kutoka nchi za Falme za Kiarabu na KS Energy ya Uturuki huku mkataba mwingine ukisainiwa na Kampuni ya ESSA ya nchini Indonesia kwa ajili ya uzalishaji wa mbolea aina…

Read more →
12
Sep

BODI YA WAKURUGENZI TPDC YAKAGUA MIRADI YA CSR

Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wakiongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bw. Dismas Fuko wamekagua miradi ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) iliyofanywa na TPDC katika Kijiji cha Msimbati, Mtwara. Miradi hiyo ni ujenzi wa Kituo cha Polisi na Kituo cha afya Kijiji cha Msimbati ambapo Kituo cha Polisi kipo zaidi ya 98% kukamilika na Kituo cha afya kipo 90% kukamilika ili…

Read more →
10
Sep

SERIKALI KUVUTIA WAWEKEZAJI UTAFUTAJI WA MAFUTA NA GESI NCHINI

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Serikali itaendelea kuvutia wawekezaji katika tafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi nchini ili Watanzania wanufaike na rasilimali zilizopo. Dkt.Biteko ameyasema hayo leo tarehe 10.09.2024 wakati wa hafla ya makabidhiano ya leseni ya uendelezaji eneo la ugunduzi wa gesi kati ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na ARA Petroleum katika kisima cha Ruvuma Ntorya mkoani Mtwara.…

Read more →
09
Sep

MIRADI YA GESI ASILIA KUWANUFAISHA WANANCHI

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema kuwa dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha Wananchi wananufaika na miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye maeneo yao. Mhe. Kapinga amesema hayo mkoani Mtwara wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyolenga kukagua visima vya kuzalisha gesi asilia katika eneo la Mnazi Bay pamoja na miradi inayofanyika…

Read more →
07
Sep

MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI TPDC ASHIRIKI KONGAMANO LA INDONESIA AFRICA

Kwa mwaliko wa Serikali ya Indonesia, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC Mhe. Balozi Ombeni Sefue, alihudhuria Kongamano la Indonesia-Afrika mjini Bali Indonesia. Pamoja na kushiriki katika mjadala na Viongozi wengine, Balozi Sefue pia alishiriki katika hafla ya makabidhiano ya Hati ya Makubaliano (MOU) kati ya TPDC na PERTAMINA inayoongeza muda wa ushirikiano kati ya Kampuni hizo mbili kuendelea kushirikiana katika kujenga uwezo pamoja na kutafuta fursa za uwekezaji nchini…

Read more →
21
Aug

UJENZI WA KITUO MAMA CHA GESI ILIYOSHINDILIWA (CNG) WAFIKIA ASILIMIA 33.5

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Mhe. Balozi Ombeni Sefue amesema ujenzi wa Kituo mama cha gesi iliyoshindiliwa yaani Compressed Natural Gas (CNG) umefikia asilimia 33.5 na utakamilika mwezi Desemba. Hayo ameyasema leo tarehe 21.08.2024 wakati wa ziara ya kutembelea na kujionea maendeleo ya  ujenzi wa Kituo hicho kilichopo barabara ya Sam Nujoma eneo la Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Balozi Sefue…

Read more →
15
Aug

TPDC YATOA ELIMU YA MAFUTA NA GESI ASILIA KWA VIONGOZI WA DINI NA MADIWANI

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limesema hadi sasa tayari magari 2,000 yameunganishwa na mfumo wa kutumia gesi asilimia huku nyumba 1,511 zikitumia gesi hiyo kama nishati ya kupikia. Pia taasisi zaidi ya 10 na viwanda 56 zimeunganishwa kwenye matumizi ya nishati hiyo ambayo inachangia zaidi ya asilimia 50 ya umeme kwenye  gridi ya Taifa. Unafuu wa matumizi ya gesi asilia kwenye magari unabainishwa na Mamlaka ya Udhibiti wa…

Read more →
18
Jul

TPDC YAUNGA MKONO MPANGO WA NISHATI SAFI NCHINI

‘’Ujenzi wa Kituo mama cha kushindilia gesi asilia kwenye magari (CNG) ni sehemu ya Mpango Mkakati wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha Watanzania wote wanatumia nishati safi kwenye magari, kupikia na vyombo vingine vya moto.’’ Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Dkt. James Mataragio wakati alipotembelea eneo la ujenzi wa Mradi wa Kituo MaMa cha…

Read more →
09
Jul

TPDC KUONGEZA KASI YA USAMBAZAJI GESI ASILIA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba amesema Serikali imejipanga kushirikiana na sekta binafsi katika kuongeza kasi ya ujenzi wa miundombinu ya usambazaji wa  gesi asilia majumbani,viwandani  na kwenye magari Akizungumza alipotembelea banda la TPDC kwenye Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara amesema TPDC inaendelea kutekeleza miradi hiyo ya usambazaji gesi asilia katika maeneo mbalimbali hivyo kwa kushirikiana na sekta binafsi itaweza kuwafikia watumiaji wengi zaidi Aidha…

Read more →
01
Jul

DKT.MATARAGIO AKAGUA UJENZI WA KITUO MAMA CHA KUJAZIA GESI ASILIA KWENYE MAGARI

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio amekagua kazi za ujenzi wa kituo cha kujazia gesi asilia kinachojengwa katika barabara ya Sam Nujoma mkoani Dar es Salaam na kumtaka Mkandarasi kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi kwa kuongeza rasilimali watu na vifaa.Dkt. Mataragio amesema hayo tarehe 01.01.2024 alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo. Amesema watanzania wanasubiri mradi husika kwa hamu kubwa hasa katika kipindi…

Read more →