Our Latest Blog Posts
18
Mar

WANAFUNZI WANACHAMA WA VILABU VYA MAFUTA NA GESI ASILIA VYA TPDC, WATEMBELEA MIUNDOMBINU YA GESI MTWARA

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limewezesha ziara ya wanafunzi wa vilabu vya mafuta na gesi asilia kwa shule za Sekondari  Mkoani Mtwara. Ziara hiyo imelenga kuwajengea uwezo wa kutambua rasilimali za mafuta na gesi asilia zilizopo nchini, kuwaandaa wanafunzi kuwa mabalozi wazuri wa kuisemea sekta ya mafuta na gesi asilia pamoja na kuwapa hamasa ya kusoma kwa bidii ili kuwa wataalamu kwenye sekta ya mafuta na gesi asilia…

Read more →
15
Mar

MKURUGENZI MTENDAJI WA TPDC AFANYA KIKAO NA WAFANYAKAZI

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Bw. Mussa Makame amefanya kikao na Wafanyakazi wa TPDC HQ, GASCO na TANOIL.Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 15/03/2023 Jijini Dar es salaam. Akizungumza katika kikao hicho Bw. Makame amesema Shirika limepata mafanikio mengi katika mwaka 2022, ambapo miradi mbalimbali ipo katika hatua nzuri ya utekelezaji. Miradi hiyo ni mradi wa utafutaji wa mafuta na gesi Kitalu cha Mnazi Bay Kaskazini…

Read more →
02
Mar

VITUO 9 VYA KUJAZA GESI ASILIA KWENYE MAGARI KUJENGWA

VITUO 9 VYA KUJAZA GESI ASILIA KWENYE MAGARI KUJENGWA Mkurugenzi wa Biashara ya Mafuta na Gesi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dkt. Wellington Hudson amesema jumla ya vituo tisa (9) vya kujaza gesi asilia kwenye magari vinatarajia kujegwa na kukamilika katika kipindi cha miezi 24.Dkt. Hudson ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam wakati akifanya mkutano na Waandishi wa Habari kwa lengo la kutoa ufafanuzi kuhusu changamoto…

Read more →
26
Feb

SALAMU ZA PONGEZI

Tunakupongeza Ndg.Mussa Mohammed Makame kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Read more →
24
Feb

TPDC NA KAMPUNI YA VITOL GROUP YAJADILI BIASHARA YA LNG

Menejimenti ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) imekutana na kufanya Kikao Kazi na Kampuni ya Vitol Group ya nchini Uingereza kwa lengo la kujadili biashara ya kusindika gesi asilia kuwa kimiminika (Liquified Natural Gas). Kikao kazi hicho kimefanyika ikiwa ni miongoni mwa mikakati ya Serikali kujiandaa katika kutekeleza mradi huo ambapo kwa sasa upo katika hatua za mwisho za majadiliano ya Mkataba wa Nchi Hodhi (HGA). Kampuni ya…

Read more →
10
Feb

TPDC NA ENH WASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), limesaini mkataba wa ushirikiano katika maeneo ya gesi na mafuta na kampuni ya Mafuta ya Taifa (ENH) ya nchini Msumbiji tarehe 09/02/2023 Jijini Dar es salaam. Mkurugenzi wa Biashara ya mafuta na gesi kutoka TPDC Dkt. Wellington Hudson amesema, kusainiwa kwa mkataba huo ni mafanikio ya ziara ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini Msumbiji na ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili. Mkataba…

Read more →
08
Feb

TPDC NA ENH KUSHIRIKIANA

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzani (TPDC) na Kampuni ya Mafuta ya Taifa ya Msumbiji (Empresa Nacional de Hidrocarbonetos-ENH) zimekubaliana kuanzisha ushirikiano wa kimkamkati katika sekta ya utafutaji na uendelezaji wa rasilimali za gesi asilia na mafuta.Makampuni hayo mawili yamekutana Jijini Dar es salaam kwa ajili ya majadiliano ya kushirikiana ambapo TPDC ilitoa mualiko kwa ENH kwa lengo la kuanzisha majadiliano hayo muhimu kwa nchi zote mbili.Akiongea baada ya kikao…

Read more →
07
Feb

ZAMBIA YAJIFUNZA TANZANIA KUHUSU NISHATI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati wa Zambia, Mhandisi Himba Cheelo amefanya ziara ya kutembelea mitambo ya kupokea gesi asilia  inayosimamiwa na GASCO Kampuni Tanzu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) iliyopo Kinyerezi Jijini Dar es Salaam. Akiwa katika mitambo hiyo Mhandisi Cheelo amesema,  lengo la ziara hiyo ni kujifunza namna Tanzania imepiga hatua katika suala la uzalishaji na usambazaji wa gesi asilia kwa matumizi mbalimbali. "Zambia imefanya…

Read more →