Our Latest Blog Posts
02
Apr

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA NISHATI AFANYA ZIARA TPDC

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio,amefanya ziara ya kikazi katika  Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na kuzungumza na Menejimenti ya TPDC  lengo likiwa ni kujenga uhusiano wa karibu na kuboresha ushirikiano katika sekta ya nishati. Ziara hiyo imefanyika katika Ofisi za TPDC zilizopo Jengo la Benjamin Mkapa- Posta Jijini Dar es Salaam. Ziara hiyo ilijikita katika kuelewa zaidi namna Shirika linavyofanya kazi na changamoto…

Read more →
26
Mar

NAIBU WAZIRI MKUU NA WAZIRI WA NISHATI AZINDUA RASMI KIWANDA CHA UWEKAJI MIFUMO MBALIMBALI KWENYE MABOMBA YA MRADI EACOP

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko amefanya uzinduzi rasmi wa Kiwanda cha uwekaji mifumo mbalimbali katika mabomba yatakayotumika kusafirisha mafuta ghafi mradi wa EACOP kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga Tanzania tarehe 26.03.2024. Dkt. Biteko amesema kwamba ujenzi wa Mradi huo unaendelea vizuri ambapo hadi sasa kwa upande wa eneo la kuhifadhia mafuta ujenzi wa matenki makubwa manne Chongoleani Tanga umefikia asilimia 37 huku ujenzi…

Read more →
23
Mar

PIC YAFURAHISHWA NA UWEKEZAJI WA SERIKALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imefurahishwa na matokeo ya uwekezaji uliofanywa na Serikali katika Sekta ya mafuta na gesi asilia nchini. Hayo yamejiri wakati wa ziara maalumu ya Kamati hiyo ilipotembelea mitambo ya uchakataji gesi asilia ya Mnazi bay na Madimba Mkoani Mtwara. Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Deus Sangu (Mb) alisema kuwa Kamati imefurahishwa na matokeo ya uwekezaji uliofanywa na unaoendelea kufaywa…

Read more →
20
Mar

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI (PAC) YARIDHISHWA NA MATUMIZI YA FEDHA ZINAZOTOLEWA NA SERIKALI MRADI WA EACOP

Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) imefanya ziara ya kikazi katika Kiwanda cha kuweka mifumo ya kupasha joto mabomba ya mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kilichopo eneo la Sojo Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora. Akizungumza katika Ziara hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Japhet Hasunga (Mb) alisema kuwa ziara ya kamati hiyo ililenga kuangalia mambo matatu ambayo ni; kuangalia uwekezaji…

Read more →
31
Aug

KAMPUNI TANZU ZA TPDC; GASCO NA TANOIL ZAPATA BODI ZA KUDUMU

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) leo tarehe 31/08/2023 limezikabidhi rasmi Kampuni zake Tanzu za GASCO na TANOIL miongozo na Sheria mbalimbali zitakazowaongoza katika utekelezaji wa majumu yao mapya. Aidha, Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC, Balozi Ombeni Sefue amewaasa Wenyeviti na Wajumbe wa Bodi hizo kutafsiri malengo ya Shirika mama (TPDC) yaliyotolewa na Serikali na kuhakikisha Menejimenti za Kampuni hizo zinatekeleza Majukumu yao kwa ufanisi na kuleta faida katika…

Read more →
20
Jul

TPDC KUONGEZA WIGO WA MATUMIZI YA GESI ASILIA

Mkurugenzi Mtendaji  wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Bw. Mussa Makame amesema TPDC imejipanga kuhakikisha gesi asilia inayozalishwa Nchini kwaajili ya kuzalisha nishati ya umeme majumbani  unatumika kwenye matumizi mengine ikiwemo uendeshaji wa magari. Bw. Makame amesema hayo tarehe 20/07/2023 Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na Wahariri wa Vyombo vya Habari kwa lengo la kujadili mafanikio na mikakati  mbalimbali ya Shirika kwenye utekelezaji wa miradi ya…

Read more →
08
Jul

MAKAMANDA WA JESHI LA POLISI WATEMBELEA MIUNDOMBINU YA GESI ASILIA MKOANI MTWARA

Maafisa kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Makamanda  na Wakuu wa Polisi kutoka Mikoa ya  (Dar es salaam, Pwani, Lindi na Mtwara) inayopitiwa na bomba la gesi asilia wamefanya ziara ya kutembelea miundombinu ya gesi asilia iliyoko Mnazibay na kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba mkoani Mtwara. Ziara hiyo iliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kupitia Kampuni Tanzu (GASCO) ikiwa na  lengo la Makamanda hao kujionea…

Read more →
07
Jul

TPDC, TAQA WASAINI MAKUBALIANO KWENYE UTAFITI

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na kampuni ya TAQA ya nchini Misri wamefikia makubaliano ya kushirikiana katika kufanya utafiti na kuangalia masoko ya gesi asilia katika Mkoa wa Dar es Salaam.Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi wa Idara ya Biashara ya Mafuta na Gesi kutoka TPDC Bw. William Chiome amesema, matokeo ya utafiti huo yatasaidia kuwepo kwa mipango madhubuti ya kusambaza gesi asilia kwa matumizi tofauti.“Utafiti huu utaenda kufanyika…

Read more →
25
Jun

NYUMBA 209 ZA MNAZI MMOJA MKOANI LINDI KUANZA KUTUMIA GESI ASILIA

Maafisa wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), wamefanya mkutano wa kutoa elimu kuhusu matumizi ya gesi asilia kwa Wananchi wa Kata ya Mnazi Mmoja mkoani Lindi.Lengo la mkutano huo lilikuwa ni kuwahamasisha wananchi wa maeneo hayo waliopitiwa na bomba la gesi kuwa na utayari wa kununua majiko ya gesi ili waweze kuunganishiwa gesi asilia kwenye nyumba zao kwaajili ya matumizi.Katika eneo hilo jumla ya nyumba 209 zinatarajiwa kuunganishwa…

Read more →
1 2 3 7