Our Latest Blog Posts
03
Aug

India Kuwekeza Kwenye Sekta ya Nishati

India Kuwekeza Kwenye Sekta ya Nishati Wawekezaji katika sekta ya gesi asilia na mafuta kutoka nchi mbalimbali duniani  wanakutana nchini, kwa lengo la kutafuta fursa za uwekezaji kwenye sekta hizo. Wakiwa hapa nchini pamoja na mambo mengine, wawekezaji hao wanashiriki kwenye  kongamano la nne la nishati Tanzania linalofanyika Mkoani  Dar es Salaam. Kando ya kongamano hilo la siku mbili,  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dkt.…

Read more →
02
Aug

EACOP Mambo Safi

EACOP Mambo Safi Manyara, Wakazi wa Kijiji cha Njoro Kata ya Kibaya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara wameishukuru Serikali kwa kuendeleza mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP),  kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga. Wakizungumza na Mwandishi wa  Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wakazi hao wamesema,  wako tayari kuchangamkia fursa za ujenzi katika mradi huo.  Mwalimu Clemenciana Shayo ni miongoani mwa watu  waliopisha mradi huo na…

Read more →
26
Jul

Wananchi wa Kinyagigi wafurahia Mradi  wa EACOP 

Wananchi wa Kinyagigi wafurahia Mradi  wa EACOP  Wananchi wa Kata ya Kinyagigi Singida Vijijini waliopisha mradi wa bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima, Uganda hadi Chongoleani Tanga wamesema,  wapo tayari kuchangamkia fursa mbalimbali kutokana na mradi huo. Wananchi hao wa vijiji vya Kinyagigi na Mitula katika kata hiyo ambao kwa sasa wanahakikiwa maeneo yao na mali zao wamesema,  wanafurahi kupitiwa na mradi huo na wamejiandaa kuchangamkia…

Read more →
25
Jul

Ujenzi wa Karakana ya Kupaka Rangi Mabomba Eneo la  Sojo Unaendelea 

Ujenzi wa Karakana ya Kupaka Rangi Mabomba Eneo la  Sojo Unaendelea  Shughuli za ujenzi wa Karakana ya mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) katika Kijiji cha Sojo, Nzega Mkoani Tabora uko katika hatua nzuri. Ujenzi huo unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu na kinachoendelea sasa ni wakandarasi kutoka kampuni nne tofauti wanashirikiana  kujenga kiwanda kitakachotumika kuandaa mabomba na kuyaongezea uwezo wa kutunza joto pamoja kupaka…

Read more →
24
Jul

Makamba: Mradi wa EACOP ni Salama kwa Mazingira

Makamba: Mradi wa EACOP ni Salama kwa Mazingira Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba amewatoa hofu watanzania juu ya usalama wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima Uganda hadi Chongoleani Tanga Tanzania akisema wanaopinga Mradi huo ni wanaharakati wasioitakia mema Tanzania. Waziri Makamba ameyasema hayo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi huo katika Kijiji cha Sojo Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora ambapo patajengwa…

Read more →
22
Jul

Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi Washika Kasi

Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi Washika Kasi Mradi wa ujenzi wa bomba la Mafuta Ghafi Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima, Uganda hadi Chongoleani,  Tanga unaendelea kushika kasi,  baada ya kukamilika kwa taratibu za awali za mradi huo. Akizungumza kwenye kipindi cha Jambo Tanzania  kinachorushwa na TBC, Mratibu wa mradi Bwana Asiadi Mrutu amesema,  kwa sasa kinachoendelea ni kulipa fidia kwa wananchi wanaopisha mradi huo na kuandaa vituo vikubwa na…

Read more →
22
Jul

Kagera ipo Imara Kulinda Bomba la Mafuta 

Kagera ipo Imara Kulinda Bomba la Mafuta  Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge alisema,  Mkoa huo  umejipanga kuulinda mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima,  Uganda hadi Chongoleani Mkoani Tanga. Meja Jenerali Mbuge amesema hayo wakati wa  mahojiano maalum na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Mkoani Kagera,  ambapo  amezungumzia ujio wa mradi wa bomba hilo nchini ukitokea Uganda. Alisema Mkoa wa Kagera…

Read more →
22
Jul

Ujumbe wa Uganda Wawasili Tanga

Ujumbe wa Uganda Wawasili Tanga Ujumbe wa watu 26 kutoka nchini Uganda ukiongozwa na Waziri wa Nishati wa nchi hiyo Peter Lokeri umewasili Mkoani Tanga lengo likiwa ni  kujionea maendeleo ya mradi wa Bomba la Mafuta linalojengwa kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga Tanzania. Miongoni mwa viongozi walioambatana na wageni hao ni pamoja na Balozi wa Uganda nchini Tanzania Richard Kabonero, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felichesmi Mramba…

Read more →
21
Jul

Uganda Watembelea Mradi wa Gesi Asilia Kinyerezi

Uganda Watembelea Mradi wa Gesi Asilia Kinyerezi Ujumbe kutoka nchini Uganda umeipongeza Serikali ya Tanzania na kufurahishwa na utekelezaji wa Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia Gesi Asilia wa Kinyerezi Mkoani Dar es salaam, baada ya kutembelea mradi huo. Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba wakati wa ziara ya Ujumbe kutoka nchini Uganda uliohusisha Waziri wa Nchi anayeshughulikia Maendeleo ya Madini, Wizara ya Nishati na…

Read more →
20
Jul

Wabunge wa Uganda Wajifunza Usafirishaji wa Mafuta Ghafi TAZAMA

Wabunge wa Uganda Wajifunza Usafirishaji wa Mafuta Ghafi TAZAMA Serikali kupitia Wizara ya Nishati imepokea Ujumbe kutoka nchini Uganda waliokuja nchini, kuona na kujifunza mambo mbalimbali kuhusu sekta ya Mafuta hasa usafirishaji wa mafuta ghafi kupitia Bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Tanzania hadi Zambia (TAZAMA). Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba amesema hayo wakati wa ziara ya ujumbe huo uliohusisha Wabunge wa Kamati ya Mazingira na Maliasili,…

Read more →