Our Latest Blog Posts
20
Jul

TPDC KUONGEZA WIGO WA MATUMIZI YA GESI ASILIA

Mkurugenzi Mtendaji  wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Bw. Mussa Makame amesema TPDC imejipanga kuhakikisha gesi asilia inayozalishwa Nchini kwaajili ya kuzalisha nishati ya umeme majumbani  unatumika kwenye matumizi mengine ikiwemo uendeshaji wa magari. Bw. Makame amesema hayo tarehe 20/07/2023 Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na Wahariri wa Vyombo vya Habari kwa lengo la kujadili mafanikio na mikakati  mbalimbali ya Shirika kwenye utekelezaji wa miradi ya…

Read more →
08
Jul

MAKAMANDA WA JESHI LA POLISI WATEMBELEA MIUNDOMBINU YA GESI ASILIA MKOANI MTWARA

Maafisa kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Makamanda  na Wakuu wa Polisi kutoka Mikoa ya  (Dar es salaam, Pwani, Lindi na Mtwara) inayopitiwa na bomba la gesi asilia wamefanya ziara ya kutembelea miundombinu ya gesi asilia iliyoko Mnazibay na kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba mkoani Mtwara. Ziara hiyo iliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kupitia Kampuni Tanzu (GASCO) ikiwa na  lengo la Makamanda hao kujionea…

Read more →
07
Jul

TPDC, TAQA WASAINI MAKUBALIANO KWENYE UTAFITI

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na kampuni ya TAQA ya nchini Misri wamefikia makubaliano ya kushirikiana katika kufanya utafiti na kuangalia masoko ya gesi asilia katika Mkoa wa Dar es Salaam.Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi wa Idara ya Biashara ya Mafuta na Gesi kutoka TPDC Bw. William Chiome amesema, matokeo ya utafiti huo yatasaidia kuwepo kwa mipango madhubuti ya kusambaza gesi asilia kwa matumizi tofauti.“Utafiti huu utaenda kufanyika…

Read more →
25
Jun

NYUMBA 209 ZA MNAZI MMOJA MKOANI LINDI KUANZA KUTUMIA GESI ASILIA

Maafisa wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), wamefanya mkutano wa kutoa elimu kuhusu matumizi ya gesi asilia kwa Wananchi wa Kata ya Mnazi Mmoja mkoani Lindi.Lengo la mkutano huo lilikuwa ni kuwahamasisha wananchi wa maeneo hayo waliopitiwa na bomba la gesi kuwa na utayari wa kununua majiko ya gesi ili waweze kuunganishiwa gesi asilia kwenye nyumba zao kwaajili ya matumizi.Katika eneo hilo jumla ya nyumba 209 zinatarajiwa kuunganishwa…

Read more →
30
May

TPDC MPISHI ASIEONEKANA HADHARANI LAKINI CHAKULA CHAKE HULIWA NA KUFURAHIWA NA WENGI

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limetajwa kama mpishi anaepika chakula kitamu na kizuri kinachofurahiwa na kupongezwa na wateja ambapo sifa hupewa mhudumu aliyehudumia chakula hicho. Hayo yamesemwa tarehe 30/05/2023 na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Bw. Mussa Makame wakati akimuelezea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa kuhusu mchango wa TPDC katika kuzalisha umeme unaotumika nchini alipotembelea Banda la TPDC kwenye Maonesho ya Wiki ya…

Read more →
19
May

TPDC YAFANYA BONANZA KUKUZA UJIRANI MWEMA

Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania limefanya Bonanza la ujirani mwema katika Kata ya Mnazi Mmoja iliyopo Mkoani Lindi  ambayo inapitiwa  na miundombinu ya bomba la gesi asilia. Bomba la kusafirisha gesi asilia  mkoani Lindi limepita katika Vijiji/Mitaa kadhaa ambayo wananchi wake wanahusika kuilinda na kuitunza miundombinu hiyo. Bonanza hilo la michezo lililoandaliwa na TPDC lilizishindanisha timu nne za mpira wa miguu kutoka Kata ya Mnazi Mmoja mbazo ni timu…

Read more →
18
Mar

WANAFUNZI WANACHAMA WA VILABU VYA MAFUTA NA GESI ASILIA VYA TPDC, WATEMBELEA MIUNDOMBINU YA GESI MTWARA

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limewezesha ziara ya wanafunzi wa vilabu vya mafuta na gesi asilia kwa shule za Sekondari  Mkoani Mtwara. Ziara hiyo imelenga kuwajengea uwezo wa kutambua rasilimali za mafuta na gesi asilia zilizopo nchini, kuwaandaa wanafunzi kuwa mabalozi wazuri wa kuisemea sekta ya mafuta na gesi asilia pamoja na kuwapa hamasa ya kusoma kwa bidii ili kuwa wataalamu kwenye sekta ya mafuta na gesi asilia…

Read more →
15
Mar

MKURUGENZI MTENDAJI WA TPDC AFANYA KIKAO NA WAFANYAKAZI

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Bw. Mussa Makame amefanya kikao na Wafanyakazi wa TPDC HQ, GASCO na TANOIL.Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 15/03/2023 Jijini Dar es salaam. Akizungumza katika kikao hicho Bw. Makame amesema Shirika limepata mafanikio mengi katika mwaka 2022, ambapo miradi mbalimbali ipo katika hatua nzuri ya utekelezaji. Miradi hiyo ni mradi wa utafutaji wa mafuta na gesi Kitalu cha Mnazi Bay Kaskazini…

Read more →